tETESI zA uSAJILI bARANI uLAYA: Barcelona yakaribia kumpata mbadala wa Neymar.....#share
On Sunday, Mundo Deportivo imeripoti kuwa Barcelona wametuma ofa
yao ya kwanza kwa ajili ya kutaka kukamilisha dili la uhamisho wa Ousmane Dembele.
Tangu taarifa kutoka kuwa Neymar ataihama Barcelona kwenda
PSG, Mchezaji huyo wa klabu ya Borussia Dortmund amekuwa akihusishwa kuhamia Barcelona.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20
amecheza dakika 90 katika kombe la German Super Cup baina ya Borussia Dortmund dhidi ya Bayern Munich jana.
Katika mchezo huo Dortmund ilipoteza kwa penati. Dembele alitoa
pasi ya mwisho kwa Pierre Emerick Aubameyang na kufunga goli la pili.
Aidha taarifa zinaeleza Barcelona imeshafanya makubaliano
binafsi na mchezaji huyo ambaye yupo tayari kuhamia klabu hiyo ya nchini
Hispania.
Kuondoka kwa Neymar ni dhahiri kwamba mchezaji huyo atakuwa na namba ya uhakika katika
kikosi cha kwanza cha Barcelona.
Aidha Barcelona imemtaarifu Dembele kuwa ni chaguo lao la
kwanza kwa ajili ya kuziba pengo la Neymar.
Kikwazo kikubwa katika dili hili ni kwamba klabu ya Borussia
Dortmund haipo tayari kumuuza chini ya Euro zinazokaribia milioni 100.
No comments:
Post a Comment