uCHAGUZI tFF: Selasela Mgombea Umakamu wa Rais aja na Sera ya Soka Bora fursa ya Ajira...#share
MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Robert Selasela amesema atakapochaguliwa katika nafasi
hiyo mkakati wake mkubwa ni kuhakikisha anaisimamia vizuri kamati ya fedha.
Kauli hiyo ameitua leo jijini Dar es Salaam akizungumza na
waandishi wa habari, amesema sera yake katika uchaguzi huu ni ‘Soka Bora Fursa
ya Ajira’, lengo ni kuufanya mpira kuwa ajira.
Amefafanua kuwa ili mpira nchini uweze kwenda mbele ni lazima
kuwepo na usimamizi wa mipango ya fedha na uchumi.
“Nimeamua kugombea baada ya kujitathimini na kuona nafaa katika nafasi
hii, naamini nitaongoza vizuri kamati hii,” amesema Selasela.
Aidha amesema lengo la kusimamia kamati hiyo ni kutokana na
kwamba matumizi mazuri ya fedha yatasaidia katika kuwekeza chini na kuinua
vipaji ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya soka.
Amesema kwa kufanya hivyo itaweza kukuza mpira na pia
kutengeneza ajira kwa vijana. Alibainisha akipata nafasi hiyo ataweza kuwa
kiungo na serikali pamoja na kumshauri Rais wa TFF katika kuweka mipango mizuri
kwa ajili ya maendeleo ya mpira.
Amebainisha pia atahakikisha mpira wa wanawake unakuwa nchini
kwani soka la wanawake Afrika Mashariki liko chini. Ameeleza katika hilo
atasimamia katika utawala bora ili kufanikiwa.
Aidha amesema katika uongozi wake atashauri TFF kujiimarisha
kwanza kisha kushuka chini katika vyama vya mpira vya mikoa na wilaya kwani
ndiko vipaji vilipo badala ya kuangalia tu ligi kuu.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment