Mfanyabiashara Yusuf Manji, wenzake 3 wahojiwa polisi kwa agizo la Mahakama...Baada ya mahojiano wapelekwa....#share
JESHI la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam leo limefanya mahojiano na Mfanyabiashara Yusuf Manji na
Wenzake watatu juu ya tuhuma zinazowakabili za Uhujumu Uchumi kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
ilivyoliagiza Jeshi hilo kumhoji.
Baada ya Jeshi hilo
kumaliza mahojiano yao dhidi ya mshtakiwa Manji na wenzake wamewakabidhi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama ilivyoamriwa Jana.
Mbali na Manji ambaye
ni mfanyabiashara maarufu nchini, washitakiwa wengine waliokabidhiwa ni Meneja
Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza
stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
Akiwakabidhi watuhimiwa
hao, wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi
Mkuu, Huruma Shaidi kuwa washtakiwa hao wamerudishwa mahakamani kama
ilivyoamuriwa, baada ya polisi kumaliza kuwahoji.
Baada ya washtakiwa
kukabidhiwa wakiwa salama na afya zao nzuri, Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo
itaendelea na utaratibu kama ulivyokuwa awali, ambapo itatajwa September
8/2017.
Jana mchana mahakama
hiyo iliruhusu Manji na wenzake kwenda kuhojiwa na Polisi ili kukamilisha
upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment