Baada ya Manji jana kufutiwa kesi na DPP, Gwajima naye leo aibwaga Jamuhuri Mahakamani Kisutu....#share
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima amefutiwa kesi ya kushindwa kutunza
silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru
arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Akisomewa kesi hiyo ya
mwaka 2015 leo akiwa na wasaidizi wake
watatu, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
alithibitishia umma kwa kusema kutokana na ushahidi wa upande wa mshitakiwa
(Askofu Gwajima) akiulinganisha na ushaidi upande wa Mashitaka(Jamhuri), haoni
sababu ya hukumu juu ya Askofu Gwajima.
Hakimu ameitaka Jamhuri kurudisha begi na silaha anayoimiliki
Askofu Gwajima mara moja.
Kufutwa kwa kesi hiyo ni ishara kwamba Gwajima ameibwaga Jamhuri.
No comments:
Post a Comment