TRL Yafuta Kwa Muda Safari za Treni ya Abiria kutoka Dar es Salaam Kwenda Mwanza na Kigoma...#share
KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL), imefuta safari ya treni ya
abiria kwa siku mbili ili kufanya marekebisho ya uboreshaji wa miundombinu ya
reli katika eneo la kati ya stesheni ya
Morogoro na Mazimbu kutokana na daraja lililopo katika eneo lenye ukubwa wa kilimeta 209/7 kuharibiwa na mvua.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Focus Sahani, alisema safari zilizofutwa ni ya Septemba 19
treni ya kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na Kigoma pamoya na ya Septemba 21
mwaka huu kutoka Kigoma na Mwanza kenda
Dar es Salaam.
Aidha ameeleza kuwa daraja hilo lilisombwa na maji ya mvua
mnamo Mei 13 mwaka huu majira ya saa 5 usiku na likafanyiwa matengenezo ya
dharura tu lakini kwa sasa tathmini ya kiufundi imefanyika na kuthibitisha kuwa
ni hatari kuendelea kupitisha treni bila kuimarisha zaidi.
“Uongozi wa kampuni umeona ni muda muafaka sasa kulifanyia
marekebisho madhubuti nay a uhakika ili kuhakikisha usalama wa wateja wetu na
wananchi kuwa unapewa kipaumbele,” amesema Sahani.
Sahani amebainisha kutokana na hali hiyo na ili kufanya kazi
kwa umakini wamelizamika kufanya marekebisho hayo ya ratiba kwa ajili ya kutoa
nafasi ya kufanikisha zoezi hilo la kulifanyia matengenezo madhubuti daraja
hilo.
Amesema ratiba nyingine zitabaki kama kawaida hadi hapo
watakapotangaza vinginevyo. Wanachi waliombwa kuzingatia hilo na kuwaunga mkono
ili waweze kuendelean kutoa huduma zao kwa uhakika na usalama unaostahili.
Na Abrahama Ntambara
No comments:
Post a Comment