MAHAKAMANI KISUTU: Watathmini wa almasi, Archard Kalugendo na Edward Rweyemamu wafikishwa mahakamani kwa kuisababishia Serikali hasara..#share
WATATHMINI wa Serikali wa almasi, Archard Kalugendo na Edward
Rweyemamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusababisha serikali hasara ya
Sh bilioni 2. 4.
Washitakiwa hao ambao ni Mkurugenzi wa Tathmini na Mthamini
wa madini, wamesomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage
na Wakili wa serikali, Paul Kadushi.
Kadushi amedai kuwa kati ya Agosti 25 na 31, mwaka huu maeneo
ya Dar es Salaam na Shinyanga wakiwa watathmini wa serikali walisababisha
hasara ya dola za Marekani 1,118,291.43 sawa na Sh bilioni 2,486,396,982.
Kadushi amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika
wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Mwijage amesema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote
hadi DPP akiamua liendelee mahakamani hapo au la.
Pia amesema masuala ya dhamana sheria kama zilivyo
inafikiriwa na mahakama Kuu hivyo mawakili watafuatilia.
No comments:
Post a Comment