Lowassa amjulia hali Tundu Lissu Hospitalini Jijini Nairobi.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Mwanasheria wa CHADEMA na Rais wa TLS Mhe.Tundu Lissu hospitalini jijini Nairobi leo hii ili kumjulia hali.

Edward Lowassa baada ya kufika Nairobi nchini Kenya na kuonana na Tundu Lissu wodini, pia alipata wasaa wa kukutana na kubadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe, Mke wa Tundu Lissu Wakili msomi Bi.Alicia Lissu na Dereva wa Mhe.Lissu Bw.Adam Simon.

Aidha baada ya mazungumzo hayo ya kina, Lowassa aliandika maneno haya "Earlier today I paid a visit at Nairobi Hospital to see our Mp, President Of TLS and dear friend Tundu Lissu. He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying", kwenye ukrasa wake wa Twitter.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search