Jeshi la Polisi la Laua Majambazi watatu Dar....#share
JESHI la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja ya bastola aina ya
BERRETA maeneo ya Mbuki Chamazi yenye namba A065775Z ikiwa na Risasi tano ndani
ya magazine katika kufuatia majibizano ya risasi kati ya akari na majambazi
wapatao watano.

Hayo yamebainishwa leo
na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari,
amesema silaha hiyo waliipata baada askari kupata taarifa ya kuwepo kwa
njama za majambazi hao watano kufanya uporaji katika maduka ya M-Pesa/Tigopesa
katuika eneo hilo, na hatimaye kuweka mtego ambapo askari walifanikiwa kuwaona
majambazi hao wakishuka kwenye gari yao kwa ajili ya kufanya tukio hilo.
“Mnamo tarehe 13/09/2017 majira ya 21:00hrs huko maeneo
ya kwa Mbiku Chamazi tulifanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya BERRETA
yenye namba A065775Z ikiwa na risasi tano ndani ya magazine katika majibizano
ya risasi kati ya askari polisi na majambazi wapatao watano,” amesema SACP
Mambosasa.
Aidha ameeleza baada ya
majambazi hao kufika eneo la tukio na kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari
walianza kufyatua risasi kuwashambulia askari na ndipo askari walipojibu
mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu kati ya watano huku
wengine wawili wakikimbia.
Amebainisha kwamba silaha
hiyo ilipopekuliwa kati ya risasi tano zilizokuwa ndani ya magazine moja
ilikuwa chemba tayari kwa kutoka huku maganda sita ya silaha hiyo(pistol)
yakipatikana eneo la tukio.
Majambazi waliojeruhiwa
walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali ya taifa Muhimbili ili kupatiwa
matibabu, Msako mkali unaendelea kuwatafuta majambazi wawili waliokimbia.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment