Breaking: David Mataka wa ATCL na wenzake yawakuta mazito Mahakama ya Kisutu muda huu.. Hakimu awahukumu miezi sita jela kila mmoja au faini mil. 70... #share
Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na Elisafi Methew ambaye ni kaimu ofisa mkuu kitengo cha fedha umethibitisha mashtaka bila kuacha shaka yoyote dhidi ya wawili hao,na hivyo kuwatia hatiani kulipa faini ya jumla ya Sh 70 milioni ama kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka sita jela.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa alimuachia huru mshtakiwa mwenzao, William Haji ambaye alikuwa mkaguzi mkuu wa Hesabu za ndani ATCL baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka dhidi yake.
Hata hivyo iliamuru Mattaka na Elisafi kulipa hasara waliyoisababishia hasara ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo in USD 143,442.75 ndani ya mwezi mmoja.
Washtakiwa hao walitiwa hatiani katika mashtaka sita yaliyokuwa yakiwakabi likiwamo la kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara.

No comments:
Post a Comment