Breaking: Lissu atoka Central Police...Kumuona Kada Chadema wa Chato aliyeko Mahabusu tangu Agosti 21 mwaka huu....#share

Na Mh Tundu Lisu.
Makamanda wote salaam.
Nimetoka Central Police Station Dar muda huu.
Kuna kamanda wetu wa Chato amewekwa mahabusu tangu tarehe 21 mwezi uliopita. Jina lake ni Obadiah Frank Kiko.


Anaelekea ni maarufu katika siasa za mitandaoni na mnaweza kumwangalia kwenye facebook page yake 'Frank Kiko' au 'Frank K. Kiko.'

Kosa lake linadaiwa la mtandao. Anadaiwa kamsema vibaya Prof. Kabudi na timu yake ya makinikia.

Alikamatiwa kwao Chato baadae akahamishiwa Geita, Mwanza na, tangu Ijumaa iliyopita, yuko Central Dar.

Hadi sasa amenyimwa dhamana ya polisi na hajafikishwa Mahakamani.

Inaelekea kosa limekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya connection ya Chato.

Kuna watu wanafikiria watapandishwa vyeo wakikamata watu wa CHADEMA, hasa wa Chato.

Kamanda huyu hana mtu anayemfahamu hapa Dar na hana msaada hata wa chakula.

Nawaombeni makamanda wa Dar mfanye utaratibu wa kumpelekea chakula mahabusu. Masuala ya uwakili niachieni mimi.

Naombeni mpaze sauti zenu ili Kamanda Obadiah aachiliwe huru au afikishwe kortini kesho.

Haya matumizi ya hovyo ya mamlaka ya kipolisi tutayamaliza kwa kuyapigia kelele muda wowote yanapojitokeza.
Wasalaam.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search