Ofisi ya Msajili wa Hazina yabaini madudu katika utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma..Asilimia 25 haiendani na mipango...#share
OFISI ya Msajili wa Hazina imebaini asilimia 25 ya tathmini
ya utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma katika eneo la mipango mikakati
haiendani na bajeti zinazoanishwa na mashirika na taasisi hizo kwa mwaka
kusababisha kutofikia malengo yaliyojiwekea.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Hazina
Dk. Oswald Mashindano wakati wa Mkutano wa utiaji saini mikataba ya kiutendaji
kati ya ofisi hiyo na mashirika na taasisi hizo zaidi ya 30.
Amebainisha kuwa uchambuzi wa tafiti wa mikataba iliyoingiwa
mwaka 2014/15 na mashirika 71 imebaini udhaifu huo unasababisha majukumu na
mipango kutokelezeka kikamilifu.
''Ofisi imebaini katika mikataba iliyopita uchambuzi wa
taarifa iliyoandaliwa tumeliona hilo ndio ndio maana mikataba hii tunaitilia
mkazo katika meaneo ya usismamizi wa rasilimali watu, fedha na utawala bora,''
alisema Dk. Mashindano.
Dk. Masindano amesema hadi sasa mashirika na taasisi 265
zimeshasaini mkataba huo huku akisisitiza kiasi kikubwa cha fedha kinatumika
kwenye uwekezaji, manunuzi na malipo ya mishahara.
Ameongeza kuwa mbali na changamoto hiyo uchambuzi umebaini wa
taarifa hiyo umebaini viashiria vya utendaji vilivyoanishwa haviwezi kupimika
kwa mujibu wa kazi zilizoanishwa na mashirika yaliyokwisha ingia mikataba.
Amefafanua kuwa bado maeneo ya usimamizi wa rasilimali watu,
fedha na utawala yapo chini ya asilimia 10 kutokana na kutosimamiwa ipasavyo na
kwamba ukusanyaji wa mapato hautiliwi mkazo.
Pia amesema mashirika mengi yalipata asilimia 17 kwenye eneo
la utoaji huduma akibainisha kuwa kazi zilizoanishwa na mashirika haziko kwenye
mpangilio ya bajeti.
Aliwahimiza watendaji kuzisimamia vyema mashirika na taasisi
zao kwenye utoaji huduma bora na kukusanya mapato yatakayoisaidia Serikali
kuendeleza miradi yake.
Ameyataja miongoni mwa mashirika na taasisi zilizosaini
mkataba huo ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) Mamlaka ya Mawasilaino
nchini (TCRA), Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Chuo Kikuu cha Ushirika-Moshi,
Shule ya Sheria nchini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Udsm) na Tume ya Vyuo
Vikuu nchini(TCU).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya Anne Makinda amewashauri watendaji wa mashirika na taasisi zilizoingia
mkataba huo kutekeleza majukumu yao ili kuchochea ustawi wake.
Na Hussein Ndubikile




No comments:
Post a Comment