Breaking News: CCM kimetoa kauli juu ya kupigwa Risasi kwa Lissu... Kimelitaka Jeshi la polisi kuwabaini na kuwashughulika haraka wahusika...#share
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kushambuliwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Mchana wa leo.
Taarifa iliyotumwa kwa Umma na Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, kimelaani tukio hilo la kikatili na lisilo na utu.
Aidha kutokana na tukio hilo wamelitaka Jeshi la Polisi kuwatafuta, kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuchukua hatua kali za kisheria kwa waote waliohusika na kitendo hicho kisicho cha kibinadamu.
Na Abraham Ntambara




No comments:
Post a Comment