Dk. Kigwangalla akana kuwa na Ugomvi na Kikwete, adai wahunzi wa maneno kujenga ukuta baina yao....#share


Naibu waziri wa AfyaMaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla ameeleza kuwa haoni ajabu yoyote kwa Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kupinga mtazamo wake na wala haimanishi kwamba wawili hao wanaugomvi.



Kauli hiyo imekuja  baada ya hivi karibuni Dkt. Kigwangalla kuweka ujumbe katika ukurasa wake wa twitter akitoa maoni yake juu ya usaili wa awamu ya kwanza kwa wanaotafuta ajira katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliyofanyika Agosti 30, 2017 na kupelekea Mbunge Ridhiwani Kikwete naye kutoa maoni yake juu ya hicho jambo ambalo watu wengi walihisi pengine wawili hao wanachukiana kwa namna moja ama nyingine.

Kutokana na mabandiko hayo ndipo Naibu waziri huyo wa afya Dkt.Kigwangalla naye alipoweza kujitetea kwa upande wake juu ya tukio zima jinsi lilivyotokea.

"Naona wahunzi wa maneno wanaanza kujenga ukuta kati yangu na Ridhiwani kikwete. Sioni nia mbaya kwenye 'comment' yake na wala sina kinyongo naye!.Siyo ajabu mimi na mtani wangu Ridhiwani ama mwanaccm yeyote yule kuwa na mitazamo tofauti kwenye suala la ajira, hiyo haimaanishi tuna ugomvi", aliandika Dkt. Kigwangalla.

Pamoja na hayo, Dkt. Kigwangalla aliendelea kwa kusema
"viongozi wa CCM (wenye dola) ni vizuri tukijadili suala la changamoto ya ajira kwa sababu tuna nafasi ya kushawishi suluhu ndani".


Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangalla amesema katika changamoto kubwa ambazo viongozi wa leo wanakupambana nazo ni pamoja na suala zima la ajira.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search