Itel Mobile Yasherehekea Maadhimisho Ya Miaka 10 Kwa Mafanikio Makubwa...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

ITEL Mobile leo imesheherekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake huku itel ikiwa ni moja ya kampuni vinara kwa ubora Barani Afrika.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Itel Leslie Ding, amesema katika kipindi cha miaka 10 itel imeonesha nguvu ya mabadiliko tangu kuingia kwenye soko la Afrika kwa mwaka huu wa 2017.

“Hii ni kutokana nan a baada ya kuanzishwa kwa timu ya watu wenye ujuzi na moyo wa kufanya kazi. Miaka 10 sasa, itel imekua na imeenea Zaidi ya nchi 45 duniani kote. Tunaamini kuwa tuna timu imara ambayo hata mafanikio ya miaka 10 iliyopita ni kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na timu hii,” amesema Ding.

Aidha ameongeza kuwa katika kipindi hicho itel mobile imekuwa na mabadiliko chanya ya bidhaa kutokana na kufuata matakwa ya wateja wake.

Ding ameongeza kuwa kampuni hiyo kwa sasa inapendwa na watu wengi na inamvuto kutokana na bidhaa zao kuboreshwa zaidi kwa ubunifu mkubwa ambapo wameweza kuongeza wateja mara mbili zaidi barani Afrika na kwamba hadi sasa wameweza kuuza simu milioni 100.

Amesema pia mafanikio hayo yamechangiwa na kushirikiana na mastaa wan chi za Afrika kama mabalozi wa kampuni yao na kwamba wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni hiyo ambayo ni miongoni mwa kampuni tatu bora barani Afrika.

Aliongeza kuwa wanaposherehekea miaka 10 wanatarajia nguvu yao ya mabadiliko itakuwa kubwa zaidi na wanaendelea kuliimarisha bara la Afrika kwa kutoa bidhaa bora zaidi za mawasiliano.

Naye Balozi wa Itel nchini Irene Uwoya ameipongeza kampuni hiyo kwa ubora wake ulioifanya kuwa miongoni mwa kampuni tatu bora za barani Afriaka.
Kwa upande mwingine Itel Mobile imezindua simu mpya za kisasa ambazo ni itel S12 na S32.

Akizungumzia simu hizo Ofisa Masoko  wa Itel Saiphon Asajile alisema simu hizo ni bora na zina kamera mbili za kuweza kupigia selif mbili za picha.

Pia katika hafla hiyo kampuni hiyo imetoa tuzo kwa washirika ambao wameweza kufanya vizuri katika biashara na kuchangia mafanikio ya kampuni.













Na Abraham Ntambara


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search