Maye wa Ubungo Chadema Aendelea Kumng'ang'ania "Bashite"..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

MEYA wa  Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema hayuko tayari kukaa meza moja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumaliza shauri la kesi alilofungua Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma la kutumia vyeti feki linalomkabili mkuu wa mkoa huyo badala yake anataka shauri hilo lifikishwe Baraza la Maadili ukweli ujulikane.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meya Jacob baada ya kumaliza kuhojiwa na sekretarieti hiyo jijini humo.

Amesema katika mahojiano hayo amewasilisha hoja zake za msingi bila kupingwa ila cha kushangaza Sekretarieti ilimuambia hata yeye ana kesi ya kujibu kutokana na mkuu wa mkoa huyo kuwasilisha tuhuma zinzoeleza Jacob aliwahi kutumia ofisi za manispaa hiyo kwa shughuli za kichama kitu ambacho si kweli.

" Nashukuru katika hoja zangu zote nilizowasilisha hakuna iliyopingwa ila nimeshangaa kuingiziwa hoja ya kutumia ofisi ya manispaa kichama sikufanya bali nilitembelewa na Frederick Sumaye," amesema meya Jacob.

Amebainisha kuwa tuhuma hizo hazimvunji nguvu za kuendelea kuhakikisha Makonda anafikishwa mbele ya baraza hilo kujibu shtaka lake na kwamba hata Chama cha Mapinduzi kimeshawahi kutumia Ikulu kufanyia shughuli za chama hicho.

Meya Jacob amesema hata jana (juzi) CCM ilitumia ukumbi wa Ikulu kufanya Mkutano wa Kamati Kuu jambo ambalo si halali kisheria huku akionyesha picha zinaonyesha wajumbe wakiwa kikaoni.

Amesisitiza kuwa endapo itapatikana vithibitisho kuwa alitumia ofisi hizo kufanyia shughuli za chama hana kipingamizi kwa sekrtarieti hiyo kufanya kazi  kama sheria zinavyoelekeza.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria zinavyolekeza sekretarieti hiyo inatakiwa kuchukua hatua mara tu inaposikia tuhuma za kiongozi na sio mpaka isubiri mtu aende kushtaki.

Aidha, amesemema shtaka jingine ni Makonda  kula kiapo kwa kutumia vya majina yasiyo yake mbele ya rais kwani kufanya hivyo kudanganya mamlaka ya rais.

Ameongeza kuwa hafanyi hivyo kumkomoa Makonda bali anakata kuona hatua zinachukuliwa na ukweli ubainike kwa yale aliyoyashtaki kwenye sekretarieti.

Meya Jacob amesema ana mashahidi wa kutosha wakiwemo watu waliosoma na Makonda na Walimu waliowahi kumfundisha.

Pia amesema anataka Makonda atumie jina la Daudi Albert Bashite lilopo kwenye vyeti vyake na si vinginevyo na kwamba hata ikibainika mkuu wa mkoa huyo ni darasa la saba atakuwa tayari kufanya naye kazi bila ubaguzi wowote.

Hussein Ndubikille

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search