sPORTS nEWS: Timu za Ligi Kuu, Draja la Kwanza Hatarini Kutupwa Nje ya Mashindano....#share
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limetaka hadi kufikia Septemba 22 mwaka huu, klabu zote 16 za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na 24 Ligi Daraja la Kwanza (FDL), ziwe
zimekamilisha taratibu za kupata Leseni za Klabu, zikishindwa zitaondolewa
katika mashindano.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na TFF leo, kupitia kwa Ofisa Habari wake, Alfred Lucas, Kamati ya Leseni za
Klabu imebainisha kuwa timu tano za Ligi Kuu ya VPL kati ya 16 hazikuchukua fomu za maombi ya
Leseni za klabu, huku 11 zikichukua na kurejesha lakini zina upungufu mkubwa
katika kukamilisha vigezo.
Kamati ya Leseni za Klabu
imekutana zaidi ya mara tatu katika vikao na kujiridhisha kwamba kwa ujumla
vigezo vifuatavyo havijakamilika kwa asilimia 100 katika klabu nyingi kama
zifuatavyo:
1. Klabu zote hazina programu ya
kuendeleza mpira kwa vijana.
2. Taarifa za klabu haielezi
kuhusu miundombinu ya kuhudumia walemavu wakati wa mchezo.
3. Klabu hazijaonesha uwanja wa
mazoezi.
4. Hazijaambatanisha mikataba ya
watendaji kama vile Katibu Mkuu; Ofisa Usalama wa timu, Mhasibu au mkurugenzi
wa fedha, na daktari n.k.
5. Taarifa hazina maelezo ya kocha
wa timu za vijana.
6. Klabu hazijajaza fomu za
kuomba Leseni ya klabu.
7. Hazijambatanisha katiba ya
klabu.
8. Klabu hazijaambatanisha ripoti
ya fedha ya mwaka.
9. Klabu hazijajaza fomu ya
kuthibitisha kushiriki mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Taarifa hiyo imesema, Kamati ya
Leseni ya Klabu inazitaka klabu kukamilisha vigezo hivyo kabla ya Septemba 22,
mwaka huu. Vinginevyo, klabu inaweza kuondolewa kwenye mashindano.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment