Kamanda Mambosasa aweka hadharani sababu kumshikiria Rungwe kwa siku 9...Aachiwa kwa dhamana Usiku mnene...#share

POLISI Kanda Maalim Dar es Salaam imeeleza sababu za kumshikiria mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe ambaye jana aliachiwa kwa dhamana baada ya kusota mahabusu kwa siku nne.


Mwanasiasa huyo ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), alishikiriwa kwa siku tisa akituhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Kanda hiyo,  Lazaro Mambosasa amesema polisi ilimkamata mwenyekiti huyo wa Chaumma tangu Agosti 28 baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa  mlalamikaji Suleiman Ysian (48) na mwezake Ali Riza Belgen ambao ni mfanyabishara na Raia wa Uturuki aliyefika nchini kwa biashara ya kununua korosho.

“Raia hao wa kigeni walielezea jeshi la polisi  nia yao ya kununua korosho kiasi cha tani 15 kwa mwenyeji wao Salum Mohamed ambaye aliwahakikishia kuwa kampuni yake inauwezo wa kuwauzia, na kuandaa mkataba na kampuni ya Les tropiques group mining sprl limited” alisema.

Amesema baada ya makubaliano hayo muuzaji  huyo wa korosho aliwajulisha kumshirikisha wakili wake katika makabidhiano hayo ya fedha, ambapo walikwenda hadi kwa wakili Rungwe ambaye alishuhudia makabidhiano hyo.

“Muuzaji alimtaka mteja wake atume malipo ya awali ya kuaandaa korosho kupitia Benki ya CRDB kwa kutumia akaunti ya wakili wake Hashimu Rungwe, kiasi cha USD 72,000 sawa na sh.milioni 160 za kitanzania, ambazo zingelipwa kwa awamu tatu na  mwisho  mzigo ambapo ungefika wangemalizia asilimia 60” alieleza Kamanda Mambosasa.

Amesema kuwa mfanyabiashara huyo akiwa Uturuki  Novemba 22, 2016  alituma fedha kiasi cha zaidi ya sh.milioni 20 kwenye akaunti ya Wakili na sh.milion mbili  kama gharama za kwenda Lindi kuhakikisha mzigo kama hupo.

Hata hivyo baada ya uthibitisho huo kutoka mtuhumiwa huyo Novemba 12, mwakajana alitumiwa kiasi cha zaidi ya sh.milion 30 katika akauti  ileile, hivyo mteja alipoona gharama zinazidi kuwa kubwa na hakuna mzigo alimua kurudi Uturuki akisubili kutumiwa.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search