Chadema Kimelituhumu Bunge kuvunja Katiba kwa Kuomba Fedha za Ziada Nje ya....#share

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai Bunge limevunja Katiba kwa kuomba fedha za ziada nje ya bajeti yake iliyoidhinishwa na Bunge bila kupitisha maombi bungeni. 


Akizungumza na waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa chama hicho, Vicent Mashinji alisema ibara ya 135 (2) inaeleza kuwa Fedha ambazo hazijawekwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina ya serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na sheria kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum.

“Kwa mujibu sheria ya uendeshaji wa Bunge mwaka 2008, kifungu cha 31 kinaeleza kuwa fedha zote kwa ajili ya uendeshaji  wa bunge zinawekwa kwenye mfuko maalum wa bunge kama ulivyoanzishwa na sheria hiyo na usimamizi mkuu wa fedha hizo ni Katibu wa Bunge kwa mujibu wa kipengele cha (2) na (3),” amesema.

Amesema kati ya June 21, 2017 na Agosti 15, 2017 Katibu wa Bunge aliandika barua tatu tofauti akiomba fedha zaidi ya Sh bilioni 9 kwa waziri wa Fedha na kwa Katibu Mkuu Hazina kwa ajili ya kugharamia bajeti ya ziada na matumizi mengineyo kwa ajili ya bunge ikiwa ni nje ya bajeti iliyoidhinishwa 2016/17.

Dk. Mashinji amesema tangu wakati huo mpaka Agosti 15 serikali ilishatoa bajeti ya ziada kwa bunge sh. Biloni 7 kutoka katika mfuko mkuu wa hazina bila kufuata masharti ya katiba na kwmaba inategemewa kuwa itaendelea kutoa sh. Bilioni 2.5 kwa ajili ya kulipia gharama za posho ya jimbo ya Juni mwaka 2017 ambayo haijalipwa kwa ukamilifu.

Fedha zilizotolewa kama bajeti ya ziada zilitumika kwenye kukidhi mahitaji  ya kulipia posho mbalimbali za wabunge ya Juni mwaka 2017, posho za vikao kwa wabunge ya Mei na Juni mwaka jana posho ya masaa mengi kwa watumishi ya Mei na ya kikao kamati maalum.

Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Bunge liliidhinisha fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida sh. Bilioni 92 ambapo mishahara ni sh. Bilioni 23, matumzi mengineyo sh. Bilioni 68 na miradi ya maendeleo ya fedha za ndani sh. Bilioni 7.

Amesema kwa mujibu wa katiba ya nchi pamoja na sheria na kanuni zinazoongoza bunge na serikali ni kuwa bunge linaisimamia Serikali.

Amesema sheria ilitungwa ili bunge liwe na fedha zake kwenye mfuko maalum likiwa kama mhimili unaojitegemea na unaopaswa kujiendesha bila kuwa tegemezi.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search