Kijana Samson Peter mtuhumiwa wa utekaji wa watoto, Afariki kwa kupigwa risasi na Polisi akijaribu kutoroka..#share

KIJANA anayetuhumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto jijini Arusha, Samson Peter amefariki dunia kwa kupigwa risasi na askari polisi akijaribu kuwakimbia wakati wapo njiani kwenda kuwaonyesha washirika wenzake wa utekaji katika eneo la Muriet Mkoni jijini humo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kubainisha kwamba  mtuhumiwa huyo alipigwa risasi ya mguuni kama onyo la kujaribu kumtoroka Askari aliyekuwa ameongozana naye majira hayo ya saa 5:30 usiku.
Mkumbo amesema kuwa baada ya tukio hilo la kumjeruhi  mtuhumiwa Samson Peter kwa nia ya kumuadhibu, alifikishwa Hospital ya Mt. Meru ili kupatiwa matibabu lakini alifariki kutokana na kuvuja damu.

"Ni kweli mtuhumiwa amefariki. Ambapo jana usiku wakati alipokuwa amesindikizwa na polisi kuwaonyesha waashirika wenzake alitaka kutoroka, lakini katika hatua ya kumuadhibu kwa kitendo chake hicho ndipo akapigwa risasi ya mguuni ambapo ilimpelekea kuvuja damu nyingi na alifariki baada ya kufikishwa hospitali" amesema Kamanda Mkumbo.

Hata hivyo Kamanda Mkumbo amesema msako zaidi wa kuunasa mtandao huo bado unaendelea na iwapo wakipatikana wote watakumbana na mkono wa sheria.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search