Breaking News: Mwanasheria Mkuu Chadema Tundu Lissu apigwa risasi....#share

Tundu Lissu amepigwa risasi.


Chanzo:Mbunge Marwa Ryoba wa Serengeti kupitia ukrasa wake wa facebook, amsema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amepigwa Risasi.


Lakini hajaeleza chanzo cha kupigwa kwake "Lissu amepigwa risasi" ameandika

Aidha Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kupigwa  risasi kwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma.

Amesema kwa sasa Lissu amepelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupatia matibabu huku akieleza hali yake kuwa mbaya sana.


“Ni kweli amepigwa risasi akiwa nyumbani kwake, na sasa yupo katika hospitali ya mkoa Dodoma, naomba uniache kwa sasa,” amesema Mbowe akiongea na ITV mda mfupi uliopita.

Na Abraham Ntambara 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search