Lissu leo amafika Mahakamani Kisutu kwa kesi ya Dikteta 'Uchwara'...Mvutano mkali wa kisheria watokea baina ya mawakili wa serikali na wa Lissu...Hakimu aahirisha kesi na kutoa siku 14....#share
RAIS wa Chama cha
Mawakili wa Tanganyika (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu leo
amefika mahakamani Kisutu kwenye kesi inayomkabili ya ‘Dikteta Uchwara.
Aidha mara tu baada ya
kufika mahakamani hapo upande wa mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kuwa imefunga ushahidi katika kesi ya hiyo ya Lissu.
Mutalemwa Kishenyi ambaye
ni wakili wa serikali amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo
imeitishwa kwa ajili ya ushahidi lakini wamemaliza ushahidi.
Baada ya kueleza hayo,
Lissu amesema wakili wake Peter Kibatala hayupo, isipokuwa anawasilisha hoja
kwamba hana kesi ya kujibu. Hata hivyo, wakili Kishenyi amedai kuwa hakuna
kipengele kinachoruhusu mshtakiwa kusema hana kesi ya kujibu ama lah.
Kutokana na hatua hiyo,
Lissu amedai kuwa hoja za upande wa mashtaka sio sahihi, kwa sababu kifungu cha
230 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinatoa nafasi kueleza kama kuna kesi ya
kujibu ama hakuna.
“Hivyo tunaomba tupate fursa kwamba kwa ushahidi uliopo katika recodi
hakuna kesi ya kujibu,” amesema Lissu.
Hata hivyo, wakili
Kishenyi amesema kwa kusisitiza kuwa hakuna kifungu cha namna hiyo, hivyo
mahakama itoe uamuzi kama ana kesi ya kujibu ama lah.
Kutokana na mvutano
huo, Hakimu Mwambapa amesema anakubaliana na hoja za upande wa mashtaka kwamba
hakuna kifungu kinachomruhusu mshtakiwa kueleza kama ana kesi ya kujibu ama
lah, isipokuwa ana haki ya kuieleza mahakama.
Hakimu Mwambapa amesema
anatoa siku 14 kwa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao September 18/2017 na
October 4/2017 atatoa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu ama hana.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment