TMA imetoa leo mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba...Pia imezitaka sekta zinazohusika na hali ya hewa....#share

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za vuli na  mifumo ya hali hiyo katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu na athari zake huku ikizitaka sekta mbalimbali zinazohusiana na hali ya hewa kujiandaa kutelekeza majukumu yake.


Sekta hizo ni kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanyamapori, maliasili na utalii, nishati na maji, mamlaka za miji, afya na Menejimenti za maafa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na mvua hizo.

Amebainisha kuwa katika kipindi hicho mvua zinatarajiwa kuwa za wastani katika maeneno mengi ya mikao ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha huku akisistiza utabiri wa maeneo mengine yaliyosalia utatolewa mwezi Oktoba.

''Mvua za chi ya  wastani na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hususan katika mikoa iliyotajwa pamoja na maeneo ya Visiwa vya Unguja na Pemba,'' amesema Dk. Kijazi.

Dk Kijazi amesema kuanzia mwezi Septemba hadi Oktoba maeneo ya Ziwa Viktoria, ukanda wa pwani yatapata mvua za vuli na kwamba Novemba Nyanda za Juu Kaskazini Masahariki mvua zitanyesha eneo hilo.

Ameongeza kuwa ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba ikiendana na vipindi virefu vya ukavu vikitarajiwa kujitokeza Oktoba.

Amefafanua kuwa mvua hizo kanda ya ziwa mvua hizo zitaanza maapema kati ya wiki ya pili na tatu ya Septemba na kusambaa katika mikoa ya Geita, Shinyanga,  ifikapo wiki ya tatu na ya nne ya mwezi huo huku zikitarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba.

Pia amesema Nyanda za juu kaskazini Mashariki mvua hizo zitaanza wiki ya pili  na ya tau ya mwezi Novemba zikitarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani akibainisha zitaisha wiki ya nne ya mwezi Disemba.

Dk. Kijazi amesema hali ya joto la juu ya wastani iliyopo magharibi mwa Bahari ya Hindi inatarajiwa kuendelea katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba.

Amewashauri wakulima na wafugaji kuvuna maji kwa ajili ya matumizi ya baadaye pamoja na wachimbaji madini kuwa makini na ongezeko la maji linaloweza kusababisha maporomoko.

Aidha, amezishauri mamlaka hizo kuhakikisha mifumo ya maji inafanya kazi ipasavyo ili kupeusha maji kutuama na kwamba wananchi wameshauriwa kujikinga na magonjwa ya milipuko.

Katika hatua nyingine ameishauri menejimenti hiyo kuhakikisha inatunza mazingira, matumizi mazuri ya ardhi na mipango miji pamoja na maandalizi hatua stahiki zinazotakiwa kuchukuliwa kutokana na madhara ya mvua.

Na Hussein Ndubikile


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search