MAHAKAMANI KISUTU: Mfanyabiashara Yusuf Manji aibwaga serikali ya JPM... Aishi Keko kwa miezi...#share


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi Mkuu Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati akionyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Manji na wenzake.
Mwenyekiti huyo wzamani wa Klabu ya Yanga na wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali.

Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine.

Kuachiwa huru kwa Manji dhidi ya kesi hiyo ni kwamba sasa atabaki akikabiliwa na kesi moja tu ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo bado iko mahakamani.

Aidha kuondolewa kwa kesi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mfanyabiashara huyo kuporwa na Serikali ardhi ya ekali 712 eneo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Unaweza kusema Manji amekuwa katika misukosuko kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kuishi katika gerezani.


Na Mwandishi wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search