SPIKA Ndugai ajibu mapigo kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amtaka kuieleza....Hayo aliyosema...#share
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mbunge huyo wa Arusha kumlaumu Spika Ndugai kuwa ameshindwa kutetea kiti chake, kwa kuzidi kuwakandamiza wabunge wa upinzani hususan suala la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.
Spika Ndugai akizungumza leo wakati akiendesha bunge, amesema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalolihusu bungeni.
"Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai
Aidha Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge.
"Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyopelekwa Lissu", amesema Spika Ndugai.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amesema anamsamehe Godbless Lema na kuwataka watu kumsamehe kwani hajui alitendalo.
Na Mwandishi Wetu




No comments:
Post a Comment