Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Awataka Majaji na Mahakimu Kupambana na Rushwa...Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan
amewataka Majaji na Mahakimu kupambana na rushwa katika mahakama ili
kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfurulizo ambapo kauli mbiu ya Mkutano huo ni 'Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi'.Mkutano huo umehudhuriwa na majaji pamoja na mahakimu wa nje mwanachama wa Jumuiya ya Madola.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar
es Salaam wakati akifungua Mkutano mwaka wa siku tatu wa Majaji na Mahakimu wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais
John Magufuli.
Aidha amesema kuwa rushwa huondoa
uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sharia.
“Niwatake washiriki wa mkutano huo
kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo
vinapatikana,” amesema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amepongeza mafanikio
makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa
Jumuiya ya Madola (CMJA).
Amesema ” Jitihada zenu katika
kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza
utawala wa sheria vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara
zaidi”.
“Kwa miaka mingi mmeendelea
kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza utawala
wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola,” amesema Makamu wa Rais.
Aidha, mkutano huo uliohudhuriwa na
Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa
Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini
na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli. “Naamini kwamba nia ya kujenga
mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya
Tanzania itajitenga na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”,
alisisitiza Makamu wa Rais.
Amewahakikishia
washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuheshimu na
kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa kuhakikisha inaendelea kupambana na
kuondoa vitendo vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa
mkutano huo, Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Ignasi Kitasi
amesema moja ya changamoto inayowakabili ni ufinyu wa bajeti inayoelekezwa
kwenye shughuli za mahakama unachangia kukwamisha utoaji huduma na utendaji wa
mahakama katika kusguhulikia mashauri mabalimbali.
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Ignasi Kitasi akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Majaji na Mahakimu wa Nchi za Jumuiya ya Madora leo Jijini Dar es Salaam (Picha na Abraham Ntambara)
Amesema kutokana ufinyu wa
rasilimali fedha mahakama zimekuwa zikishindwa kukamilisha majukumu yake kwa
wakati mwafaka huku akisisitiza ufinyu huo husababisha malalamiko kutoka kwa
wananchi wenye madai na kesi ambazo ziko mahakamani.
" Changamoto kubwa
inayoikabili mahakama bdao bajeti inayotengwa ni finyu tatizo hili linapelekea
shughuli za utendaji kutofanyika ipasavyo likiwekewa mkazo naamini malalamiko
yatapungua," amesema Kitasi.
Amefafanua kuwa mahakama nchini
zinaendelea kufanya kazi bila kuingiliwa huku akiongeza mkutano huo umebeba
kauli mbiu inayohimiza kujenga mahakama shirikisha inayowajibika.

Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Dar es Salaam kwa siku tatu Mfurulizo Mkutano huo unakauli mbiu inayosema 'Mahakama Madhubuti, inayowajibika na Jumuishi'.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Majaji pamoja na mahakimu wanawake waliohudhuria mkutano Mkuu wa Mwaka wa Majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola Unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment