Waziri Ummy Apiga Marufuku Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Kutoa Rufaa kwa Matibabu ya Nje..Habari Kamili Hii Hapa na Matukio360..#share

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha haitoi rufaa ya matibabu nje ya nchi kwa maradhi ambayo wana uwezo wa kuyatibu nchini.

Image result for waziri ummy mwalimu

Ummy amesisitiza wataalamu kutowaogopa wanasiasa ikiwa wana uwezo wa kumtibu mgonjwa hapa nchini haina ulazima wa kumwandikia rufaa nje ya nchi hata akiwa ni Rais John Magufuli.

Ametoa agizo hilo leo Jumatatu wakati akipokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba viwili vya upasuaji vya watoto wadogo na wodi ya watoto ya upasuaji vyenye thamani ya Dola za Marekani 675,000 sawa na Sh1.5 bilioni,  kutoka kwa wataalamu na wahisani kutoka nchini Uingereza kupitia taasisi ya Archie Wood Foundation.

"Rais aliponiteua aliniagiza kwamba lazima niachane na rufaa za nje, hatuwezi kuachana nazo ikiwa magonjwa yanayoweza kutibiwa ndani yatatibiwa nje," amesema Ummy.

Amesema Watanzania wana imani na  Muhimbili  na hivi sasa wengi wanatoka hospitali za kulipia na kufuata matibabu ila changamoto iliyopo ni majengo lakini wapo mbioni kujenga jengo la ghorofa kwa ajili ya wagonjwa wa kulipia.

"Msitoe rufaa ya mgonjwa kama hamjajiridhisha kwamba mnaweza kumtibu hapa hata kama awe Rais, waziri au nani msitoe rufaa kwani maana yake mtakuwa mmeshindwa ni lazima ninyi mseme kwamba hamuwezi na sisi tutashughulikia," amesema.

Amewatahadharisha wataalamu hao na wanasiasa kwamba lazima wahakikishe kweli hawawezi kutibu na kwamba wizara ipo tayari na itawaunga mkono.

Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search