Mbunge Kubenea Aiwashia Moto Serikali Kufungiwa Gazeti la Mwanahalisi..Naibu Waziri wa JPM Kumlipa Mamilioni..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
BAADA ya wiki moja kupita tangu serikali kulifungia kwa mwaka
miaka miwili gazeti la Mwanahalisi, kwa madai ya kuwa Gazeti hilo linaandika
habari zinazokiuka kanuni za uandishi wa habari,Wamiliki Gazeti hilo wameibuka
na kuipa siku mbili serikali kulifungulia gazeti hilo kabla ya kwenda
mahakamani.

Pia wamesema endapo serikali ikikataa ombi lao watamfungulia kesi
binafsi Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo
Anastazia Wambura ya kumdaib fidia ya milioni 41 kwa kila chapisho la
gazeti ambalo litakuwa halitoki tangu kufungiwa kwa madai sheria haijampa
mamlaka ya kulifungia gazeti.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam, na mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Puplishers Limited ,Saed Kubenea wakati wa
mkutano na waandishi wa habari amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini
kuwepo na uonevu wakati wa kulifungia gazeti hilo.
“Tumewaandikia barua hawa watu kuwa ndani ya siku mbili
walifungulie Gazeti hili,na kama wakikaidi mwanasheria yupo hapa tunakwenda
kufungua kesi binafsi kwa Naibu waziri ,tunataka watulipe hela hii
ya milioni 41 moja ya kila toleo la gazeti ambalo alitoki ikiwa ni hasara
aliotuingizia” Amesema Kubenea.
Kubenea ambaye ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) amesema hata
hatua ya serikali kuliifungia gazeti la Mwanahalisi ni kuidharau muhimili
wa mahakama kutokana na Mahakama kuu kutoa umuzi wa kutoguswa gazeti
hilo.
“Leo tunashangaa serikali hii inapuuza uamuzi wa
mahakama ambao ulitaka gazeti hili lisiguswe kwa namna yeyote,maana Jaji
alisema kama waziri akitaka kuligusa gazeti hili anatakiwa kwenda mahakamani na
mahakama kutoa maauzi,lakini tunashangaa leo wanakuja kulifungia gazeti”
“Na hata ukiangalia barua ya kufungia gazeti hili,imesainiwa
na Naibu waziri wakati sheria ya Huduma ya habari ya 2016 imemtaja Waziri na
sio naibu waziri,pia sheria hiyo haimpi waziri kulifungia gazeti bali
inamtaka kuzuia tu maudhui sio kufungia gazeti”amesema Kubenea.
Naye Mwanasheria wa Kampuni hiyo,Fredrick Kiwelo amesema kwa
sasa wameshamwandikia notsi ya siku mbili Naibu waziri kuondoa zuia la
kulifungia Gazeti.
“Hawa tumewashaaandikia barua,huku tujiandaa kwa taratibu
zengine za kufungua kesi za kudai fidia maana kumetokea ukiukwaji mkubwa kwenye
kulifungia kesi’Amesema Kiwelo.
KUHUSU TUHUMA ZA GAZETI LA MWANAHALISI
Kubenea ambaye ni Mwandishi Nguli wa habari nchini kwa sasa,
amesikitishwa na maelezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa habari Maelezo,Dkt
Hassan Abasi kuwa gazeti la mwanahalisi limekuwa likiandika habari za kutunga
na zenye kukiuka kanuzi na misingi ya taaluma na habari.
Kubenea amesema maelezo ya Mkurugenzi huyu ni ya kupuuzwa
kwani gazeti lake limekuwa likiandika habari za ukweli.
“Hili Gazeti linaendeshwa na watu weledi kwenye vyombo vya
habari si vyeti tu bali wanauadilifu mkubwa wa kimaadili,leo miongoni mwa
wahariri wa gazeti hili ni, Nyaronyo Kichele huyu alikuwa ni mhariri wa gazeti
la Kulikoni ambalo hapa Abassi ndipo alipofanya kazi,sasa leo walimfundisha
kazi huyu Abassi leo ndio wanaandika habari za uongo?”Amehoji kubenea.
Mbunge huyu Mchachali amesema kwa sasa kinachoisumbua
serikali kwa sasa ni kutokana na wamiliki wa gazeti hilo kukataa “kuilamba
miguu serikali”
"Nataka ni waambieni tulipofungia mara ya kwanza mwaka
2012 kutokana na kuandika habari ya kutekwa,kupigwa na kutupwa kwa kiongozi wa
madaktri nchini Dk Steven Ulimboka,tulimtaja mtu mmoja anaitwa Ramadhan Igondu
kuwa nahusika ,na hata serikali hakuna mahala popote walipokanusha kuhusu huyu
mtu na hata Dk Ulimboka alikuja na kukiri kumfahamu huyu mtu na akamtaja
nahusika ,"
"Na hata tulipokwenda mahakamani serikali ikatufungulia gazeti ,sasa leo unaposema gazeti hili linaandika habari za uongo ni vipi"ameendelea kuhoji.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment