Meya Jacob Abaini Mchezo Mchafu Sakata la Vyeti Feki vya "Bashite"...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

TUME  ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia kumhoji Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob kuhusu  madai yake aliyowasilisha kwa tume hiyo akitaka Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwamba ameghushi vyeti vya shule. 
Jacob amesema kuwa tume hiyo imemtaka afike ofisini kwao kesho asubuhi ili aweze kutoa maelezo juu ya mashtaka yake juu ya Makonda.

Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Ubungo amesema ameitwa kupitia barua yenye kumbukumbu namba  CAG 31/37/01/42.

Hata hivyo, Jacob amesema kuwa tayari kuna viashiria vya vishawishi vya yeye kuachana na shauri hilo linalomkabili Makonda.

Mwezi Machi mwaka huu  Jacob aliwasilisha mashtaka manne katika tume hiyo pamoja na moja la  jinai ambalo ni la kughushi  vyeti vya taaluma.

Hivi karibuni Makonda alipachikwa jina la Bashite ambalo linadaiwa ndilo jina lake halisi alilopewa na wazazi wake.


Na Mwandishi Wetu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search