Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo awaonya Chadema kugeuza mtaji wa kisiasa shambulio la Tundu Lissu.. #share
MKUU wa majeshi ya Ulinizi na Usalama nchini Jenerali Venance Mabeyo ameshtushwa na namna Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wananvyoweka uzito mkubwa katika tukio la kushambuliwa kwa Tundu lissu.
Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari, amesema kitendo cha kupigwa risasi Rais huyo wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) limefanywa kuwa tukio kubwa kuwahi kutokea wakati kuna matukio makubwa kama ya Kibiti ambayo yaliyoathiri na kuua watu wengi na vyombo vya usalama viliachwa kufanya kazi yao.
‘kwanini matukio ya kibiti hayaleti mstuko mkubwa sana sasa wakati watu walioathirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa?’ amehoji Jenerali mabeyo.
Aidha Jenerali Mabeyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuviacha vyombo vya dola kufanya kazi yake kwani kwa sasa vimeingia kazini.
Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ameahidi kuwa wahusika wote watawatia nguvuni na hali itakuwa shwari.
Na Mwandishi Watu

No comments:
Post a Comment