Zitto Kabwe akwama tena kwa Spika Ndugai,.. “tutakwenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke.." #share

MBUNGE wa Kigoma Mjini
(ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe
amemjibu Spika Job Ndugai kuwa
ameibua mashitaka yake ili ku￾funika ufuatiliaji wa wananchi
kuhusu hali ya Mbunge wa Sin￾gida Mashariki, Tundu Lissu.


Zitto aliandika majibu hayo
jana mchana muda mchache
baada ya Spika Ndugai kueleza
kuwa anaweza kumzuia kuzun￾gumza bungeni kwa muda wote uliobaki.
Alibainisha kuwa amegundua
Ndugai ameibua mashitaka dhidi
yake, ili kufunika ufuatiliaji wa
wananchi kuhusu Lissu kupigwa
risasi.
Jana asubuhi bungeni Dodoma,
Spika Ndugai alisema anaweza
kumpiga marufuku Zitto kuzun￾gumza bungeni kwa kipindi cho￾te cha Bunge la 11 na hana cha
kumfanya.
Spika alitoa kauli hiyo siku
moja tangu alipompeleka Zitto
kwenye Kamati ya Haki, Kinga
na Madaraka ya Bunge kwa kud￾harau Bunge.
Akizungumza jana baada ya
kipindi cha maswali na majibu,
Ndugai alisema anaweza kuli￾chambua Bunge, kwa sababu
alikuwapo katika vipindi hivyo,
na Anne Makinda na marehemu
Samwel Sitta ni walimu wake.
“Hawa ni watu nawaheshimu
sana na wamenilea sana na mpa￾ka sehemu nilipofika leo. Utanil￾inganishaje mimi na milima mi￾kubwa kama Kilimanjaro? Hata
siku moja, sikio haliwezi kuzidi
sikio,” alisema.
Alibainisha kuwa katika Bunge
la Tisa, Zitto alipeleka hoja ya
Mgodi wa Buzwagi ambayo
ilikataliwa na Bunge, lakini ika￾zuka hoja ya kimaadili na alihu￾kumiwa hapo hapo.
“Alihukumiwa hapo hapo aka￾pigwa miezi mitatu. Mnataka
niende mkuku kama Bunge la
Tisa nifanane na Mzee Sitta? Hilo
pia naliweza kwa nini mnaalika
matatizo, nashangaa unapamba￾na na Spika,” alisema.
Alisema ana uwezo wa kupiga
marufuku kuzungumza hadi
miaka yote mitano na Mbunge
huyo wa Kigoma Mjini, akose pa
kuongelea na hakuna swali lolote
atakalouliza na kumtaka kupam￾bana na watu wengine, lakini si yeye.
“Kwa haya ya Spika sina sababu
nayo, lakini ya kulidharau Bunge
hayo sitayavumilia, nitalinda
mhimili huu kwa nguvu zangu
zote,” alisema.
Alisisitiza hawawezi kuacha
wabunge kulidhalilisha Bunge na
kuhoji watachukuliaje Watanza￾nia wengine watakapolidhalili￾sha Bunge.
Alisema kwa kuwa hilo ni kosa
la pili kwa Zitto, ameagiza apele￾kwe katika Kamati ya Maadili,
“tutakwenda sambamba mguu
kwa mguu hadi kieleweke.”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search