Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney kukumbana na Rungu la Koeman kwa Utovu wa nidhamu..#share
WAYNE Rooney atakutana na mgogoro mkubwa atakapokutana na
kocha wake Ronald Koeman wiki hii na
huenda akakabiliwa na adhabu kutoka kwa meneja huyo.
Nahodha huyo wazamani Uingereza alipewa onyo kabla ya kujiunga
kwa mara nyingine na klabu ya Everton kwa
kuambiwa na Koeman kuwa ni lazima kwa kila mchezaji wake kuishi nidhamu.
Lakini Rooney, ambaye alikamatwa na polisi ijumaa iliyopita kwa
kumuendesha mtoto wa kike nyumbani kwake huku akiwa amelewa atajumuishwa katika kikosi kwa kuwa kocha alishindwa
kusajili mshambuliaji mwingine wa kati katika dirisha lililofungwa.
Ukweli ni kwamba Koeman kwa sasa anamuhitaji Rooney, hususani
katika michezo ya lighi ya Europa inayokuja.
Koeman alizungumzia maswala ya pombe katika
mkutano mrefu na Rooney kabla ya kumsaini, baada ya kuonya juu ya matukio
yanayohusiana na kunywa pombe ambayo yamepunguza ubora wa kiwango chake.
Koeman alihakikishiwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa timu
ya Manchester United kuwa hatarudia tabia hiyo ya ulevi.
Pamoja na tabia hiyo ya Rooney ni ukweli kwamba meneja wake anavutiwa na mtazamo wa mchezaji na jinsi anavyojituma katika mazoezi na wakati wa mechi.
Kama Rooney atapewa adhabu na Koeman hatakuwa mchezaji wa
kwanza kuadhibiwa na kinidhamu na Meneja huyo kwani wliowahi kupewa adhabu ni
pamoja na Zlatan Ibrahimovic akiwa Ajax and Santiago Canizares akiwa Valencia.
No comments:
Post a Comment