Ripoti ya hali ya Tundu Lissu... Katibu Mkuu Chadema Dk. Mashinji asema hali yake bado siyo nzuri sana... Madaktari bado wanaendelea kuokoa maisha yake #share


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hali ya Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu bado si ya kuridhisha.


Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa Chakula Di.  Vincent Mashinji, amesema Lissu ameshafanyiwa oparesheni tatu na inaonesha alipigwa risasi zaidi ya tano.

"Kuanzia jana asubuhi, Lissu alianza kusikia maumivu ya kifua, mguu wake wa kulia umevunjwavunjwa na kwa risasi," amesema.

Aidha amebainisha kuwa Mguu wa kulia wa Lissu ulivunjwavunjwa zaidi ya mara 3 au mara 5, pia nyonga na mkono vilivunjwa kwa risasi.

Amesema risasi hizo pia zilimvunjavunja mguu wa kushoto pamoja na nyonga ambapo hadi sasa ameongezwa damu nyingi.

 Amebainisha kwamba jana hali yake ilibadilika na kuwa mbaya , akawa anapumua kwa mashine, lakini madaktari walifanya kazi kubwa, hivyo leo ameamka salama.

Ameongeza kwa sasa madaktari wanahangaika kuunganisha mifupa yake iliyovunjwa kwa na kueleza kwamba watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo apone.

 Alivyoondoka walikuwa  hatujui kama atarudi mzima kwani alikuwa na hali mbaya na walikuwa tayari kupokea hali yoyote na ingekuwa ni zawadi waliyopewa na Mungu.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search