Tucta yajitosa kupigwa risasi kwa Lissu.. Yasema alifanyiwa kitendo cha Kihuni....#share
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania
(Tucta), Dk.Yahya Msigwa amelaani kitendo cha kihuni cha kupigwa kwa risasi
mchana kweupe Mbunge wa Singinda Mashariki, Tundu Lisu.
Matukio mengine ambayo hayatakiwi kufumbiwa macho ni pamoja
na utekaji raia, utekeji watoto wadogo na mauaji kwa baadhi yao, mauaji ya
kijambazi ya watu wasio na hatia, Kibiti, Mkuranga na Kilwa.
Dk. Yahya ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Amesema Tanzania
tumezoea kuwa kisiwa cha amani na kutofautiana kwa hoja na fikra na kujijengea
utamaduni wa kupinga bila kupigana
kuamini kuwa hoja inajibiwa kwa hoja.
"Kitendo hicho kimetushtua raia wa Tanzania na
Ulimwanguni kote, hivyo vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza wajibu wao,"
alisema.
Ameeleza vitendo hivyo visipokemewa na kulaaniwa
yatatuchafulia nchi taswira nzuri tuliyojijengea kwenye uso wa kimataifa,hivyo
TUCTA wamelaani matendo yote maovu.
Ameongeza kwa kuiomba serikali kutumia vyombo vyake vya dola
kufanya jitihada ya kuwajua wahalifu ili kukomesha matukio hayo ya kihuni
kutokea.
Aidha, amesema ili huduma au uzalishaji ufanyika katika jamii
msingi wake ni amani, iwapo amani itatoweka watu hawawezi kwenda kanisani wala
Misikitini kuabudu.
Amesema dalili zilizojitokeza zinaonesha amani yetu ipo
hatarini kutoweka iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kwa ajili ya kudhibiti.
"Tusikubali lulu ya Tanzania kupotea, hivyo tusikubali
jambo lolote kutokea kuharibu amani yetu, tuitunze na kuilinda," amesema.
Na Mwandishi Wetu



No comments:
Post a Comment