Taarifa Zaidi ya Kushikiliwa kwa Mbunge wa Geita Vijini Joseph Msukuma na Jeshi la Polisi Hii Hapa... #share

MBUNGE  wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amekamatwa na Polisi mkoani humo, kutokana na tuhuma za kuhusika kwa tukio la kufungwa kwa njia kwenye barabara ya kuelekea kwenye mgodi wa GGM wiki iliyopita.

Akithibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo alipokuwa akionga na mwandishi wa habari wa East Africa Television, amesema Musukuma amekamatwa leo baada ya kupata taarifa kuwa anahusika na tukio hilo.

"Ni kweli Mbunge Musukuma tumemkamata leo kufuatia tukio la juzi" amesema Kamanda Mwabulambo.
Pia Kamanda Mwabulambo amesema mpaka sasa wanawashikilia watu 8 ambao 6 miongoni mwao ni madiwani wa kata mbali mbali mkoani humo, na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kama ambavyo inatakiwa.

Siku ya Alhamisi ya Septemba 14, 2017, wananchi mkoani Geita walifunga barabara inayoingia katika mgodi wa GGM kushinikiza malipo ya kodi ya dola 12.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search