Zitto amcharukia Spika Ndugai..Adai Bunge limemshinda..Amtuhumu kuwasaliti huku akijua jinsi walivyompigania dhidi ya Hujuma za IKULU..#share
MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema kwa sasa heshima ya Bunge imeporomoka.
Zitto amebainisha hayo kupitia katika mtandao wake wa kijamii huku akieleza kuwa anamheshimu Spika Ndugai na kuonyesha kumsikitikia.
"Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia," amesema.
Kauli hiyo imekuja baada ya Zitto kutakiwa na Spika Ndugai kesho kufika katika Kamati ya Maadili ya Bunge kutokana na kutuhumu kuwa Bunge limewekwa mfukoni.
Ameeleza kuwa Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge akipigwa risasi lakini mkutano wa bunge ukiendelea.
Zitto amedai kuwa kwa uzoefu wao walikuwa na matumaini na spika Ndugai ambaye walimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu kuwa angewaunganisha kwa kutambua nguvu aliyonayo ili kukabili udikteta unaonyemelea nchini na asingehangaika na ukosoaji wenye staha wanaoufanya.
"Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 sasa hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge" amesema Zitto Kabwe




No comments:
Post a Comment