Zitto, Kubenea wamjeruhi Spika Ndugai...Awageukia kama Mbogo na kuwapeleka kwa pilato..#share

SPIKA wa Bunge Job Ndugai amamtaka Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Saed Kubenea kufika kesho mbele ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili kuhojiwa kwa kumtuhumu kuwa spika ni muongo.



Spika Ndugai amesema kuwa Kubenea amemtuhumu kwamba amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyia (TLS) Tundu Lissu.

Katika hatua nyingine Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chamka cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti zinazowakabili. 
                     

Tuma hizo ni kwamba Zitto anatuhumiwa kwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Na Mwandishi Wetu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search