ACT-Wazalendo wampa neno Magufuli...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na
Mwandishi Wetu
CHAMA cha ACT-Wazalendo
kimeitaka serikali ya Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Umoja wa Afrika na Jumuiya za kimataifa kuendelea na juhudi za kuleta amani
nchini Somalia.
Kauli hiyo imekuja baada ya kutokea kwa vifo vya watu zaidi ya
250 kutokana na mlipuko wa mabomu uliotokea ndani ya Lori mjini Mogadishu
nchini Somalia.
Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti kamati ya mambo ya nje
na ushirikiano wa Kimataifa wa ACT Venance Msebo amesema chama hicho kimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu hao.
Aidha mbali na vifo hivyo, watu zaidi ya 400 wamejeruhiwa
katika tukio hilo. Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na kikundi cha kigaidi
cha Al-Shabab usiku wa Oktoba 14 mwaka huu.
“Tunatoa pole kwa serikali na wananchi wa Somalia,
tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie uvumilivu na ustahimilivu katika
kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mamia ya ndugu zao,”.
Ameeleza kwamba juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili
kuepusha maafa na madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na kutokuwepo usalama
nchini humo. Somalia isipokuwa salama Afrika haiwezi kuwa salama, bila Somalia
salama hakuna dunia salama.




No comments:
Post a Comment