Tanesco yajenga kituo kipya cha kupoza umeme Lindi..Soma habari kamili na Matukio360..#share



Na Hussein Ndubikile

SHIRIKA la Umeme(Tanesco)  limetumia wahandisi na mafundi wake kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 132.
Meneja Mradi wa uboreshaji umeme Mkoa wa Mtwara na Lindi kutoka kampuni tanzu, EDCO Mhandisi Japhary Msuya akiwaongoza wahariri wa habari kutembelea kituo cha Mtwara.

Kituo hicho cha Mahumbika kilichopo Mkoani Lindi kinauwezo wa kupoza msongo wa umeme wa kilovolti 132 unaotoka mkoani Mtwara takribani kilomita 80. .

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anayeshughulikia usafirishaji umeme(Transmission), Mhandisi Kahitwa amesema  hayo leo mkoani Mtwara katika ziara yake na waandishi wa habari.

“Huu ni mwanzo mzuri kwetu tunaendelea kujenga vituo vingine na kituo kinachofuata kwenye mpango ni kile cha Kimbiji, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.” amesema.

Amesema  mradi huo wa Mtwara na Mahumbika umekamilika katika kipindi kifupi na upo katika ubora.

Meneja wa TANESCO Mkoani Lindi Mhandisi Johnson Mwigune amesema, kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Mahumbika, umesaidia kuboresha hali ya umeme.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search