Askofu Shao: Magufuli kama Mugabe..Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Zanzibar Mhashamu Agustino Shao amemfananisha Rais John Magufuli na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwa jinsi anavyochukua hatua katika kupigania maslahi ya Watanzania.
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Zanzibar Mhashamu Agustino Shao amemfananisha Rais John Magufuli na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwa jinsi anavyochukua hatua katika kupigania maslahi ya Watanzania.
Rais John Magufuli (Kulia) na Rais Robert Mugabe (Kushoto)
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema, Askofu Shao amesema hayo wakati akihubiri katika Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Porokia ya Minaramiwili, amesema Rais Mugabe alichukua hatua za kupigania maslahi ya Wazimbabwe na sasa wananachi wa nchi hiyo wameanza kuzalisha bidhaa na kuziuza nje ya nchi.
Hivyo Askofu Shao amesema hatua anazochukua Rais Magufuli kupambana na rushwa, kupigania rasilimali za Watanzania, kuimarisha nidhamu na uwajibikaji, kukabiliana na wizi na ubadhilifu wa mali za umma na kubana matumizi zinapaswa kuungwa mkono na watanzania wote.
"Hatuwezi kusema tunaimaliza rushwa wakati tunaendelea kuishi kwa kupata fedha ambazo hujazifanyia kazi, ni lazima tuishi machungu ya kuimaliza rushwa, ni lazima tuishi machungu ya kuweka uadilifu katika utendaji wetu, tusipoishi machungu hayo tutaishi dunia mbili, dunia ya rushwa na dunia ya kujenga uchumi na uadilifu wa watanzania, tukubali kujikatalia ili tuweze kupata mazuri tuliyotaka," amesema Askofu Shao.
Kwa upende wake Rais Magufuli amemshukuru Askofu Shao kwa mahubiri yake mazuri ambapo ameungana naye katika kuwahakikishia Watanaznia kuwa Serikali inachukua hatua za kupambana na rushwa na kulinda rasilimali za nchi ili ziweze kuwanufaisha wenyewe.




No comments:
Post a Comment