Aliyeua wanafunzi watano auawa...Soma habari kamili na Matukio360..#share
MTU mmja anayetuhumiwa kwa mauaji ya wanafunzi watano na mlinzi
mmoja katika shule ya Sekondari ya Lokichogio huko Turkana nchini Kenya ameuawa na
wakazi wa kambi ya wakimbizi ya Kakuma.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mtuhumiwa huyo alikuwa amekamatwa na polisi kabla ya wakazi
hao kuvamia Kituo cha Polisi cha Kakuma na kumchoma moto.
Kamanda wa Polisi wa Turkana Ronad Opili amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema mtu huyo alikamatwa kwenye kambi ya wakimbizi
ya Kakuma alipokuwa akijaribu kukimbilia Sudan Kusini.




No comments:
Post a Comment