Aweso Awataka Dawasco na Dawasa Kutatua Changamoto ya Miundombinu ya Maji..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji 
Jumaa Aweso 
leo amefanya ukaguzi wa miundombinu ya maji eneo 
la Ubungo na kujionea miundombinu hiyo ambayo mingi imepasuka na kuvujisha maji 
mengi kutokana na uchakavu au kuhujumiwa miundombinu hiyo.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza na msimamizi wa matengenezo wa DAWASCO 
Kanda ya Tabata, aliyekuwa akisimamia matengenezo katika eneo la 
Riverside, Ubungo kwenye moja ya miundombinu ya maji iliyoharibika.

Katika 
maeneo aliyopita ameweza kuona upotevu mkubwa wa maji unaotokana na mabomba 
yaliyopasuka kuvuja, na kusababisha maji mengi kupotea baada ya kuwafikia
wananchi kwa ajili ya matumizi.

Naibu 
Waziri Aweso alisema ipo haja ya kuchukua hatua na kuhakikisha miundombinu hiyo 
inafanyiwa ukarabati, ili kudhibiti tatizo la upotevu wa maji ambalo limekuwa
changamoto kubwa jijini Dar es Salaam.

“Nitaka 
na taasisi za DAWASA na DAWASCO tuweke mikakati ya kutatua changamoto hii, ili 
kuhakikisha kiwango cha upotevu wa maji kinapungua, kwa kuwa ni moja sababu ya 
wananchi kukosa maji ya uhakika, kwa kuwa mengi yanapotea baadala ya kuwafikia walengwa”, alisema Naibu Waziri.

Fundi wa DAWASCO akiendelea 
na kazi ya kurekebisha bomba lililopasuka eneo la Riverside, Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa katika eneo la Kibangu, Ubungo akikagua 
moja ya maeneo yaliyo na miundombinu mibovu ya maji.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search