Bongo Starehe: Baba Lulu awananga wanaomhukumu mwanae.. "kwanza wakati Kanumba anafariki Lulu alikuwa mdogo sana" #share

Baba mzazi wa muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amefunguka juu ya matatizo yanayomkabili binti yake, na kusema kwamba angejua mienendo yake inakoelekea angechukua hatua mapema kudhibiti.


Mzee Michael ameyasema hayo leo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba huenda malezi ambayo alikuwa anayapata na kumuacha huru zaidi kufanya akipendacho, ndio kilichomsababishia mwanaye kukutwa na maswahibu hayo.
“Kuja kwenye tasnia yake sikuona ajabu pamoja na kwamba sikujua kama angekuja kwenye tasnia hii ya usanii, tungekuwa kama wazungu.
kuangalia watoto ningegundua mapema, maana dalili zilikuwa zinaonekana tangu zamani, ndio maana nilikuwa namkazania kusoma na siku-‘favour’ sana mambo yake ya sanaa ”.
Amesema Mzee Kimemeta na kuongeza kuwa; hata tukio la kifo cha Kanumba lilitokea wakati akiwa na umri mdogo, na kuwataka watu kutomhukumu bali kuviachia vyombo husika vifanye uamuzi wake...

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search