CHADEMA: Serikali inawajua waliompiga risasi Tundu Lissu..Matibabu yake zaidi ya milioni 400..soma habari kamili na Matukio360...#share
Abraham Ntambara
CHAMA cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA) kimesema Serikali inawajua watu waliompiga risasi mbunge
Tundu Lissu mkoani Dodoma.
Mwenyekiti taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Pia kimesema hali ya
Lissu imeimarika na mpira wa hewa, chakula na yote aliyokuwa amewekea imeondolewa
na kwamba ameanza kutembea.
Kauli hiyo imesemwa
na mwenyekiti taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe jijini Dar es Salaam katika
mkutano wake na waandishi wa habari.
“Serikali inawajua wote
waliohusika na tukio la kumpiga risasi Tundu Lissu.” Amesema Mbowe
Ametaja baadhi ya
ushahidi kuwa mara baada ya Lissu kupigwa risasi kamera zote za CCTV
zilizokuwapo eneo la tukio ziliondolewa na hadi sasa hazijulikani mahala
zilipo.
“Pia lile eneo
alilopigwa risasi Lissu ni eneo la viongozi lina ulinzi lakini watuhumiwa wote
baada ya tukio waliweza kuondoka bila kukamtwa.” Amesema Mbowe
Kuhusu hali ya afya
ya Lissu, Mbowe amesema imeimarika na ametolewa mipira yote aliyokuwa amewekewa
na kwamba ameanza kutembea hadi kutoka
nje.
Mwenyekiti huyo
amesema pamoja na mambo mengine Lissu atapelekwa sehemu nyingine kwa matibabu zaidi.
“Kutokana na sababu
za kiusalama hatuwezi kuweka hadharani lakini
Lissu atakwenda kutibiwa mahala pengine ili kuhakikisha afya yake inatengemaa
zaidi.” Amesema Mbowe.
Kuhusu gharama za
matibabu, amesema yamegharimu zaidi ya milioni 400.
Pamoja na mambo
mengine Mbowe amesema kuhusu taratibu nyingine za kufanya wameiachia familia ya
Lissu.
“Sisi tumefanya kwa
nafasi yetu lakini pamoja na mambo mengine taratibu nyingine za kufanya
tumeiachia familia ya Tundu Lissu.” Amesema Mbowe




No comments:
Post a Comment