Mbunge ataka dawati la jinsia shuleni...Soma habari kamili na Matukio360..#share
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ameliomba Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani. Mbunge huyo alichangia kiasi cha sh. milioni 1 kwa ajili ya kusaidia dawati hilo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Iringa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) akiwa sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi.
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF)
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi na mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF).
Hawa ni baadhi ya wanamtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.



No comments:
Post a Comment