CUF yamvaa IGP …Yampa tano Sheikh Ponda...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Salha Mohamed
CHAMA cha Wananchi CUF kimekosoa mwenendo wa utendaji wa Jeshi la Polisi nchini.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif
Pia kimempongeza Sheikh Issa Ponda kwa kujitokeza hadharani na kuzungumzia matukio ya upigwaji risasi, mauaji na ukamataji holela unaendelea nchini.
Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma-CUF Taifa Mbarala Maharagande ameiambia Matukio360 kuwa Jeshi la Polisi linavunja katiba hususan kipengele cha uhuru wa kuandamana na kuzungumza.
“CUF hailizishwi na mwenendo mzima wa utendaji wa Jeshi la Polisi. Ukweli halieshimu Katiba, sasa kwa makusudi Jeshi la Polisi linabana na kuwanyima Watanzania uhuru wa kidemokrasia wa kuzungumza na kuandamana,”
Kuhusu Sheikh Ponda, Maharagande amesema kujitokeza kwake katika kipindi hiki ambacho Watanzania na Viongozi wengi wa Dini na Kisiasa wamejazwa woga, wale waliokuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika awamu zilizopita hivi sasa wamejitia upofu, ububu na uziwi.
‘’ CUF Inampongeza sheikh Ponda kwa kuelezea umuhimu na ulazima kwa Watanzania kuungana pamoja kutetea uwepo wa mfumo wa Haki, Demokrasia na Utawala wa Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitendo cha kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu kwa namna ya mfano wa vile alivyoshambuliwa yeye Sheikh Ponda mwaka 2013 Mjini Morogoro,
Havikubaliki na jamii ya Watanzania kwa pamoja tunapaswa kupaza sauti zetu kukemea mwenendo huu mbaya unaoanza kushamirishwa na kuota mizizi ndani ya nchi yetu .
Amesema Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini kwa ujumla, Wasomi, Waandishi wa Habari na Watanzania wote kila mmoja kwa nafasi yake hawapaswi kuridhia na kunyamaza kimya bila kukemea mabaya yanayoendelea kutokea nchini.
CUF imevitaka Majeshi na vyombo vinginje vya Dola kujielekeze kutekeleza wajibu wake kwa mujjibu wa madhumuni ya uwepo wake na kuacha kuacha kupambana na raia wema.



No comments:
Post a Comment