Habari katika picha: Waziri Makamba ateta na Balozi wa Sweden...#share


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  January Makamba (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kulia) katika kikao chake kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais  jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kilishirikisha pia wataalamu kutoka Idara ya Mazingira. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.







Balozi wa Sweden Nchini Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba mara baada ya kumtembelea hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine  Balozi amezungumzia namna ya kushirikiana katika sekta ya Mazingira.




Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Naibu Balozi wake Ulf Kallstig ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wakiwa Ofisini kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kufanya mazungumzo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search