Dk Tulia akabidhi milioni 40....soma habari kamili na Matukio360...#share
Naibu Spika wa
Bunge Dk Tulia Ackson amekabidhi hundi
ya milioni 40 zitakazotumika kwenye ukarabati wa chumba cha upasuaji na wodi ya akinamama
na watoto katika kituo cha afya cha Ruanda
Jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson akikabidhi hundi ya milioni 40.
Amekabidhi hundi hiyo
leo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla
na kwamba ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi Machi mwaka huu.
Amesema changamoto
hiyo iliwalazimisha wauguzi kutumia
rasiliamli fedha kuhamisha wagonjwa kwenda katika Hospitali ya
Wazazi Meta.
“Sitoishia hapa
nitakakikisha natatua kero zinazogusa kitengo
cha uzazi lengo ni kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungu."amesema.
Naye Amos Makalla,
amemwagiza mkandarasi anayekarabati jengo la chumba cha upasuaji na wodi ya
akinamama na watoto kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha na matumizi mabaya ya
fedha hizo
Mkandarasi wa Kampuni ya Emilet, Gilbat Mwandindile, amesema
changamoto wanayokabiliana nayo ni jingo kujengwa kwa tofari mbichi.



No comments:
Post a Comment