TMA yaeleza mwelekeo wa mvua nchini...soma habari kamili na Matukio360...#share

Hussein Ndubikile
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua  za msimu za mwezi Novemba mwaka huu hadi Aprili mwakani huku ikitahadharisha  Mamlaka za miji na wananchi kuchukua hatua za kuhakikisha mifumo na njia za kupitisha maji zinafanya kazi katika kiwango cha kutosha ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko, uharibifu wa miundo mbinu, upotevu wa maisha,  mali na magonjwa ya milipuko.

 Mkurugenzi Mtendaji TMA, Dkt Agnes Kijaza
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Dkt. Agnes Kijazi wakati akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na vipindi hivyo vya mvua.

Amesema katika Kanda ya Magharibi ikijumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba na kutawanyika katika mkoa wa Tabora wiki ya pili ya mwezi huo mwaka huu huku akibainisha zitakuwa za wastani hadi ya juu ya wastani katika maeneo mengi.

“Mvua kubwa zinatarajiwa katika maeneo mengi ya kanda ya magharibi katika kipindi cha miezi ya Februari hadi Aprili na zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Aprili,2018,” amesema.

Amebainisha kuwa  mvua kwenye mikoa ya Songwe, Mbeya, Iringa, Ruvuma zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya mwezi Novemba na wiki ya kwanza ya mwezi Desemba, 2017 zikitarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani  kwenye maeneo mengi kwa miezi ya Novemba hadi Januari mwakani.

Dkt Kijazi amesema katika kipindi cha miezi Februari hadi Aprili, 2018 mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani kwenye maeneo mengi isipokuwa machache ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambapo yanatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani zikiratajiwa kuisha wiki ya mwisho ya mwezi Aprili mwakani.

Amesisitiza kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya mwezi Novemba na wiki ya kwanza ya mwezi Desemba, 2017 na zikitarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani kwenye maeneo mengi katika kipindi cha miezi ya Novemba hadi Januari mwakani.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search