Tanzania kuimarisha ushirikiano na Uganda..Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi
na kidiplomasia baina yake na Uganda.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania Richard Tumusiime Kaonero, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Uganda nchini Tanzania, Richard Kaonero.
Amesema
Tanzania na Uganda zinauhusiano wa muda mrefu na kwamba Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya Rais John Magufuli inafarijika na ushirikiano huo.
“Tunaimani
kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha miradi
mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo ujenzi wa bomba la
gesi.”
Hivyo ametumia fursa hiyo
kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza kwenye viwanda
mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.
Pia
amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga
za wanyama.Kwa upande wake, Balozi Kaonero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa
kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda.
Pia
Balozi huyo ameiomba Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) kuanzisha safari ya kwenda Entebe nchini Uganda ili kuimarisha
usafiri kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumzia
kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Balozi Kaonero amesema Serikali ya
Uganda na Tanzania zinaundugu wa damu na kwamba wataendelea kuudumisha.



No comments:
Post a Comment