‘Harbinder Sethi mhhhh, Mahakama yasubiri ripoti ya Muhimbili’..Soa habari kamili na Matukio360..#share
Na Salha Mohamed
MSHTAKIWA katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
MSHTAKIWA katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Harbinder Sethi (Kulia) na James Rugemalira (kushoto)
Leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwendesha mashtaka mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amesema kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari na kwamba wiki ijayo Sethi atarudishwa Muhimbili kuchukua majibu ya vipimo vyake.
Wakati huo huo wakili wa mshtakiwa James Rugemalira, Respicius Didas ameieleza mahakama hiyo kuwa kuna suala la ucheleweshwaji wa upelelezi na kwamba washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Juni 19,mwaka 2017 na wapo ndani hadi sasa.
Amelalamika kuwa kila kesi ikifika mahakamani hapo upande wa mashtaka unadai upelelezi bado haujakamilika, huku wateja wao wakiendelea kukaa ndani na wanapata athari.
Akijibu hoja Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Swai amedai uchunguzi wa kesi ya kughushi unachukua muda hivyo aliomba mawakili wa upande wa utetezi wajue upelelezi bado unaendelea sheria ipo wazi katika masuala ya kughushi.
Katika kesi hiyo, washtakiwa Harbinder Singh Sethi na James Burchard Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa Kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi, kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Pia wanakabiliwa na mashtaka matano ya kutakatisha fedha pamoja na kusababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Rugemarila ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 27,2017



No comments:
Post a Comment